Rais na Mama Margaret watembelea familia ya marehemu Nkaissery

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto hii leo walimtembelea mjane wa waziri wa usalama, marehemu Joseph Nkaissery nyumbani kwake katika eneo la Karen hapa jijini Nairobi.
Katika ziara hiyo ya kuliwaza familia ya mwenda zake rais alitaja kifo cha Nkaiserry kuwa pigo kwa jamii ya wamaasai, akiahidi kuendelea kuweka jamii hiyo moyoni mwake.
Baraza zima la mawaziri lilishiriki misa ya wafu iliyoandaliwa nyumbani kwa Nkaiserry alasiri ya leo.

Tags:

Nkaissery

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories