Rais na naibu wake waimarisha mikakati ya kujipigia debe

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanazidi kuimarisha mikakati ya kujipigia debe kwa kinyanganyiro cha Agosti nane huku Rais Kenyata akiapa kutokubali machafuko ya baada ya uchaguzi chini ya hatamu yake.
Kwenye ziara yake katika kaunti ya Nyamira hii leo rais amesema kwamba tofauti za kisiasa hazifai kukithiri kiasi cha wakenya kuambulia vurugu, huku akitoa wito wa amani, kabla na baada ya uchaguzi wa Agosti nane.
Wakimbizi wa ndani kwa ndani wapatao 9000 walifaidika na ziara hiyo walipokabidhiwa zaidi ya milioni 450 kima kinachonuiwa kuwawezesha kupata makao mbadala.

Tags:

Uhuru kenyatta JUBILEE NYamira idps

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories