Rais na naibu wake wakutana na wakuu wa bunge la kitaifa

Rais Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na viongozi wakuu wa bunge la taifa katika ikulu ya Nairobi. Rais na naibu rais wamefanya mkutano na spika wa bunge la taifa Justin Muturi na kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale kabla ya mkutano wa pamoja utakaowajumuisha spika wa seneti Ken Lusaka na kiongozi wa wengi kwenye seneti Kipchumba Murkomen. Mkutano huo unaarifiwa kujadili suala la kalenda ya bunge na uteuzi wa makamati.

Tags:

ken lusaka Aden Duale justin muturi Rais Uhuru Kenyatta

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories