Rotich: Sijapokea mapendekezo ya IEBC

Muungano wa Cord unasisitiza makamishna wa tume ya uchaguzi nchini-eibc waondoke kufikia mwishoni mwa mwezi huu, kama ilivyopendekezwa na kamati teule ya bunge.

Kinara wa Cord Raila Odinga ameikosoa serikali kwa kujikokota katika utekelezaji wa mapendekezo ya kamati teule ya bunge, na kuhatarisha maelewano yaliyoafikiwa, ili kufanikisha maandalizi ya uchaguzi huru na haki. Hata hivyo, waziri wa hazina ya kitaifa Henry Rotich anadai kuwa hajapokea pendekezo lolote kutoka kwa makamishna wa iebc kuhusu fidia yao.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories