Ruto: Upinzani wameanza kuogopa kushindwa

Rais Uhuru Kenyatta amewataka wafuasi wake katika eneo la Mlima Kenya kujisajili kwa wingi kama wapigakura, ili kuondoa tashwishi yeyote kuhusu umaarufu wake, haswa baada ya mrengo wa upinzani- Cord kudai aliibiwa kura katika kinyang’anyiro cha mwaka 2013. Kenyatta aidha amewataka machifu na wasaidizi wao kote nchini kuweka mikakati ya kuwakabidhi vijana vitambulisho vya kitaifa, huku ikibainika kuwa zaidi ya vitambulisho laki nne havijachukuliwa na wenyewe. Naibu wake William Ruto naye amedai kuwa upinzani umeanza kuingiwa na kiwewe kuhusu idadi ya watu wanaojitokeza kusajiliwa kuwa wapiga kura katika maeneo yanaoshabikia Jubilee.

Tags:

Uhuru kenyatta Jubilee Party william ruto baringo Mt Kenya

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories