Safaricom yaandikisha faida ya nusu mwaka ya Ksh. 26.2B

Kampuni ya Safaricom hii leo imeandikisha faida ya shilingi bilioni 26 nukta 2 katika matokeo yake ya kipindi cha kifedha cha kati ya mwezi Aprili na mwezi Septemba mwaka huu. Faida hii inaashiria ongezeko la asilimia 9 nukta 5 ikilinganishwa na shilingi bilioni 23 nukta 9 faida iliyoandikishwa kipindi sawa na hicho mwaka jana.
Kampuni hiyo imetaja ongezo la mapato katika huduma za M-pesa na zile za data kama vigezo vikuu vya kuimarisha biashara hiyo.

Tags:

Safaricom

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories