Safaricom yaionya NASA dhidi ya kutoa vitisho


Afisa mkuu wa kampuni ya mawasiliano Bob Collymore amewataka wanasiasa kusita kuingiza masuala ya biashara na kampuni katika siasa akisema wataendelea kushirikiana na tume ya IEBC katika kandarasi ya uwasilishaji wa matokeo ya uchaguzi kwa njia ya kielektroniki. Collymore ambaye ameonekana kuulenga mrengo pinzani wa NASA ameapa kuwachukulia hatua wanasiasa husika endapo maafisa sita wa Safaricom waliotajwa na Raila Odinga watajipata taabani kutokana na ripoti kuwa walishiriki kuhujumu uchaguzi wa Agosti mwaka huu.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Sam Gituku
More by this author