Kiongozi wa chama cha NARC Charity Ngilu ameashiria kuwa huenda akajiunga na muungano wa CORD

Kiongozi wa chama cha NARC Charity Ngilu ameashiria kuwa huenda akajiunga na muungano wa CORD ili kuweza kumenyana na Jubilee katika kinyang’anyiro cha mwaka ujao. Katika mazishi ya mumewe kiongozi wa chama cha CCU Wavinya Ndeti, Ngilu aliashiria hayo na kusema kuwa uongozi wa juu wa CORD hauna wanawake na angehiari kurekebisha hayo. Haya yamejiri huku seneta wa Nairobi Mike Sonko akizomewa na kufurushwa na waombolezaji pale alipoanza kuwakosoa viongozi wa CORD.

Tags:

CORD Mike Sonko Wavinya Ndeti kathiani CHARITY NGILU

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories