Serikali kununua vitabu vya kusoma mwakani


Wanafunzi wa kidato cha kwanza watapata vitabu sita vya masomo ya lazima (core subjects) kuanzia Januari mwaka ujao kutoka kwa wizara ya elimu. Waziri wa elimu Fred Matiang’i ametangaza mwamko huo mpya akisema shule hazitapokea tena pesa za kununua vitabu kwani kumekuwa na wizi na ufujaji wa hela za mpango huo. Waziri alisema hayo alipozindua shughuli ya kutoa nafasi za shule za upili kwa watahiniwa wa KCPE mwaka huu ambapo pia alitangaza mabadiliko kadhaa katika sekta ya elimu.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Sam Gituku
More by this author