Shambulizi jingine eneo la Fafi

Maafisa watatu wa utawala wanauguza majeraha ya risasi baada ya msafara wao wa magari kushambuliwa na washukiwa wa Al Shabaab kati ya eneo la Yumbis na fafi kaunti ya Garissa.

Maafisa hao walikuwa wanaitikia wito wa shambulizi la usiku wa kuamkia leo lililopelekea kifo cha mtu mmoja na uharibifu wa mnara wa mawasiliano katika eneo la Fafi.

Msururu huo wa mashambulizi ukijiri saa chache baada ya maafisa saba na raiyaa mmoja kuuawa katika shambulizi La Al Shabaab kaunti ya Lamu.

Tags:

Al Shabaab Fafi

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories