Uchunguzi waanzishwa dhidi ya Raila kuhusu madai ya uchochezi


Taasisi tatu za serikali zimeanzisha uchunguzi dhidi ya kinara wa upinzani Raila Odinga, kutokana na matamshi aliyotoa siku ya Alhamisi katika eneo la Kajiado, kuhusiana na umiliki wa mashamba. Kiongozi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko ametangaza kuwa idara yake, tume ya maridhiano na utangamano wa kitaifa (NCIC) na kitengo cha upelelezi wa jinai zinapekua semi za Odinga, kubaini iwapo alivuka mpaka na kuchochea uhasama wa kijamii. Hata hivyo Odinga amejitetea vikali, akidai matamshi yake hayakueleweka vilivyo.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Floods exhume bodies at a cemetery

Story By Francis Gachuri
More by this author