Usalama kaskazini mashariki: Matiangi akutana na viongozi wa eneo hilo

Usalama kaskazini mashariki: Matiangi akutana na viongozi wa eneo hilo

Waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiang’i amekutana na viongozi kutoka eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi kuzungumzia utovu wa usalama katika eneo hilo.

Huku akiwa ameandamana na katibu wa wizara Karanja Kibicho, waziri alisema kuna mikakati ya kuimarisha usalama katika eneo hilo huku akiahidi kushirikiana na viongozi wa Kaskazini Mashariki.

Viongozi hao wakiwemo kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale na Gavana wa Mandera Ali Roba walikubali kushirikiana haswa kuhusu usalama, huku wakiahidi kuwahusisha wananchi kutafuta suluhu ya kudumu.

Aidha waziri wa elimu Amina Mohamed aliyehudhuria mkutano huo aliwahakikishia viongozi kuwa maandalizi ya mitihani ya kitaifa yanashika kasi.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories