Ustawi Wa Afya

Rais Uhuru Kenyatta leo amezindua mradi utakaogharimu jumla ya shilingi bilioni 38 wa ununuzi wa mitambo na vifaa vya kisasa vya matibabu vitakavyowekwa kwenye hospitali 2 zilizochaguliwa kutoka kwenye kila  Kaunti. Vifaa hivyo vinatarajia kusaidia vituo hivyo vya afya kuwa na uwezo wa kutibu maradhi mbali mbali ili kuzuia wakenya kulazimika kusafiri mwendo mrefu kutafuta matibabu. Magavana hata hivyo walisusia kuhudhuria hafla hiyo wakilezea kuwa hawajashirikishwa ipasavyo kujua ni kampuni zipi zilizopewa zabuni na mitambo hiyo itagharimu kiasi gani katika ununuzi na utunzaji.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories