

Harakati za kujipigia debe zimeshika kasi, baada ya jopo la uteuzi kuafikiana kuhusu watu watano waliofuzu kuwania uenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini-iebc.
Watano hao watahojiwa tarehe 28 na 29 mwezi huu, ili majina ya wawili kati yao yawasilishwe kwa rais, ili ampendekeze mmoja kwa uteuzi kuchukua usukani kutoka kwa ahmed issack hassan. Na kama anavyotuarifu Francis Gachuri, msukumo wa kisiasa na mipangilio ya kimaeneo ni baadhi ya vigezo vitakavyobaini uteuzi wa mwenyekiti mpya wa iebc.
Video Of The Day: Treasury allocates Ksh 4.5 B for procurement of vaccines