Vijana wa Akasha wakiri mashtaka ya ulanguzi wa mihadarati


Vijana wa Akasha wakiri mashtaka ya ulanguzi wa mihadarati

Vijana wawili wa aliyekuwa mlanguzi wa dawa za kulevya Ibrahim Akasha wamekiri mashtaka ya kuhusika na ulanguzi wa mihadarati walipofikishwa mbele ya mahakama mjini New York.

Bakhtash na Ibrahim Akasha walifikishwa mbele ya mahakama ya Southern District mjini New York ambako msimamizi mkuu wa kukabiliana na mihadarati nchini Amisi Massa alikuwepo.

Kwa mujibu wa idara ya jinai, wawili hao walikiri mashtaka ya ulanguzi wa mihadarati, kuhusika na ufisadi na kuzuia kushafirishwa kwao kutoka humu nchini na pia njama ya kutumia bunduki kuendeleza biashara hiyo.

Wawili hao pamoja na raia wa Pakistan Gulam Hussein na raia mwingine wa India walihamishwa hadi nchini Marekani mwezi Januari mwaka 2017 baada ya kuzuiliwa mjini Mombasa.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Former sports CS Hassan Wario convicted over Rio games scam

Citizen Reporter
Story By Citizen Reporter
More by this author