Vikao vya bunge kuahirishwa tena hadi kamati zibuniwe
Published on: November 08, 2017 08:15 (EAT)
Bunge la kitaifa limeahirisha vikao vyake baada ya vyama kufeli kuunda kamati za kuendesha shughuli za bunge. Muungano wa NASA umemwandikia spika wa bunge Justine Muturi na kumtaka awape hadi mwishoni mwa mwezi huu kuwasilisha majina yao. Aidha bunge limeidhinisha majina ya wabunge watano watakaoanzisha mchakato wa kubuni bunge la Afrika Mashariki.
Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke
Comments
No comments yet.
Leave a Comment