Vinara wa NASA kutangaza mwaniaji wa urais Alhamisi

muungano wa upinzani-nasa utamtangaza mgombea urais wake alhamisi ijayo, katika bustani ya uhuru. vinara wenza wa Nasa wamedokeza kuwa wameafikiana kuhusu masuala mengi nyeti, na hata kubuni mpangilio wa ugavi wa mamlaka, na kuwataka wafuasi wao kuwa watulivu, licha ya taharuki inayoibuliwa na kitendawili cha atakayepeperusha bendera. gavana wa bomet Isaac Ruto amepokelewa rasmi kama kinara mwenza wa nasa, huku kigwagizo cha viongozi wa upinzani kikisalia kile cha jubilee kufungasha virago, kwa madai ya kuzembea kazini.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories