Viongozi wa Jubilee watinga Nairobi
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamemhimiza mgombea huru wa ugavana kaunti ya Nairobi Peter Kenneth ajiondoe kwenye uchaguzi ujao, na kupiga jeki azma ya Seneta Mike Sonko, ili kufanikisha ari ya Jubilee kudhibiti uongozi wa jiji la Nairobi. Kenyatta na Ruto wamemuahidi Kenneth kibarua serikalini iwapo ataweka pembeni azma yake, huku wakielezea imani yao kuwa watasalia ikulu kwa muhula wa pili. Francis gachuri ana taarifa kamili kuhusu pilka pilka za Jubilee kusaka kura Nairobi.
Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000
Comments
No comments yet.
Leave a Comment