Viongozi wa NASA wazidi kukosoa Jubilee kuhusu SGR

Muungano wa Nasa umesisitiza ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Nairobi sio mafanikio ya chama cha Jubilee au serikali inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta. Kinara wa Nasa Raila Odinga amesema mradi wa SGR uliasisiwa, kubuniwa na kupangwa na serikali ya muungano, chini yake na rais mstaafu Mwai Kibaki, huku akidai Jubilee iliongeza gharama ya ujenzi huo kwa zaidi ya sh. 100b. Aidha, Nasa imesisitiza Jubilee haina lake pwani, licha ya msururu wa ziara za rais na naibu wake kujitwalia angalau kipande cha kura 1.7m za eneo hilo.

Tags:

JUBILEE Mombasa SGR NASA

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories