Wabunge wa ODM waunga mkono kuapishwa Odinga


Wabunge wa mrengo wa NASA wamefufua suala la kuapishwa kwa Raila Odinga huku hatua ya kutiwa saini barua inayolenga kuunga mkono kuapishwa kwa Kinara wa muungano huo Raila Odinga kama rais wa wananchi ikizinduliwa. Kulingana na baadhi ya wabunge chini ya muungano huo, hakuna mbunge yeyote atakayeshinikizwa kufuata mkondo wa kutia saini barua hiyo. Aidha WIPER imeshiriki kikao na kutangaza kuendelea mbele na mipango ya kubuniwa kwa bunge la wananchi katika eneo la Ukambani

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: NEWSNIGHT | Kalonzo quizzed over claims of support for Uhuru term extension

Story By Makori Ongechi
More by this author