Wahadhiri wa vyuo vikuu waandamana hapa Nairobi

Huku mgomo wa zaidi ya  wahadhiri 8000 katika vyuo vikuu 33 vya umma nchini  ukiingia siku ya 37, wahadhiri  hii leo waliandamana toka chuo kikuu  cha nairobi hadi wizara ya elimu kuwasilisha malalamiko yao kwa waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi.

Hata hivyo, waziri hakuwa ofisini na walipokewa na maafisa wengine wa wizara hiyo. Wahadhiri hao walisimama kwa muda mfupi mbele ya bunge ambapo walihutubiwa  na Seneta wa Kisumu Anyang Nyongo. Wahadhiri hao wameelezeaa wasiwasi wao kuhusu kasi ya mazungumzo huku wakisema pendekezo la serikali la bilioni  10 halikidhi mahitaji yao kwani linatekeleza ongezeko la asilimia 3 ya mshahara pekee. 

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories