Wajumbe wa vyama 5 wamuidhinisha Uhuru kuwania urais

Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto sasa wana idhini rasmi ya kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Jubilee baada ya kuidhinishwa na chama chao pamoja na vyama vingine vinne vinavyounga mkono muhula wa pili kwa Rais Kenyatta, kauli mbiu ikiwa “uhuru, tano tena”. Rais ambaye alihudhuria makongamano ya wajumbe wa vyama hivyo vyote aliwahakikishia wanachama kuwa hatachagua wala kubagua kati ya vyama tanzu na atazidi kuhakikisha umoja na maendeleo kwa wote. Aidha rais aliwasuta wapinzani wake walio kwenye muungano wa NASA kwa ubinafsi wa kujitafutia mamlaka badala ya kuangazia masuala yanayowahusu wananchi wa kawaida.

Tags:

Jubilee Party Rais Uhuru Kenyatta

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories