Wakaazi wa Mombasa wakadiria hasara kutokana na mvua


Wakaazi wa Mombasa wakadiria hasara kutokana na mvua

Wakaazi wa baadhi ya miji ya Mombasa wanaendelea kukadiria hasara kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kaunti hiyo, huku maeneo mengi nchini yakishuhudia mvua.

Baadhi ya shule pia zimeathirika kutoka na mvua hiyo inayoendelea kusababisha msongamano mkubwa wa magari barabarani.

Eneo la Free Town mjini Mombasa umeathirika na mvua huku wakaazi wakitafuta njia salama za kupitia angalau kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Barabara zimejaa maji huku wakaazi wakiduwaa wasijue pa kupitia, japo shughuli zao lazima ziendelee.

Kwa juma zima sasa, mvua imekuwa ikinyesha katika mji huu, sawia na maeneo mengine nchini ikiwemo kaunti ya Tana River na Nairobi.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Former sports CS Hassan Wario convicted over Rio games scam

Citizen Reporter
Story By Citizen Reporter
More by this author