Wana-NASA waishambulia vikali IEBC


Viongozi wa Nasa waliambulia kufanya mkutano wa hadhara katika ukumbi wa kamkunji mtaani Kibra hapa jijini Nairobi wakati wenzao wa mrengo wa Jubilee walipokuwa wakiskia hotuba ya rais bungeni. Nasa wamesema kuwa hawakuhudhuria kikao hicho kwa sababu Rais Kenyatta hana mamlaka yoyote ya kuitisha kikao cha bunge na kuwa jukumu hilo ni la rais atakayechaguliwa na wananchi katika marudio ya uchaguzi.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: On Viusasa, now you can download your videos and play them back later

Story By Faiza Wanjiru
More by this author