logo

Wana-NASA wakaidi amri ya Matiang’i, wasema Ijumaa ni siku ya maandamano

By For Citizen Digital

Malumbano makali yananukia kesho kati ya waandamanani wa muungano wa upinzani –NASA – na maafisa wa polisi katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu baada ya viongozi wa muungano wa NASA kupuuzilia mbali maagizo ya kaimu waziri wa usalama Dkt Fred Matiang’i kutoa maandamana katikati ya miji hiyo. NASA wanasema kuwa maandamano yataendelea kama yalivyopangwa na kuwa Matiang’i hana mamlaka ya kuwanyima haki yao ya kuandamana. Hata hivyo viongozi wa Jubilee wamemuunga mkono Matiang’i na kusema kuwa wananchi, wafanyibiashara na mali yao wana haki ya kulindwa dhidi ya uharibifu wa waandamanaji.

Also Read:

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: Showdown looms as parallel Jamhuri celebrations planned for Tuesday


By Faiza Wanjiru More by this author


Most RecentSponsored Content