Wananchi waanza kutumia usafiri wa Treni ya SGR

Siku moja baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuzindua usafiri wa treni ya kasi, treni mbili zimefanya safari leo, moja ikitoka Mombasa hadi Nairobi na nyingine ikitoka Nairobi hadi Mombasa. Treni hizo mbili ambazo zilikuwa za moja kwa moja bila kusimama katika kituo chochote zilichukua muda wa saa nne na nusu kufika zilikokuwa zikienda. Abiria waliofanya safari leo wakitaja safari hiyo kama ndege inayopitia kwenye reli. Mwanahabari wetu faiza maganga alikuwa katika kituo cha nairobi kushuhudia kuwasili kwa treni hiyo.

Tags:

SGR treni za kisasa

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories