Wanasiasa wajipigia debe wapewe nyadhifa za uaziri


Bunge huenda lisiahirishwe Alhamisi ijayo kama ilivyoratibiwa, kutokana na kibarua cha kuwapiga darubini watakaopendekezwa kuhudumu katika baraza la mawaziri. Uongozi wa bunge utakutana na Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto siku ya Jumatatu, kujadiliana kuhusu ratiba ya bunge, huku orodha ya watakaopendekezwa kuhudumu katika baraza la mawaziri ikitarajiwa kuwasilishwa bungeni juma lijalo. Na kama anavyotuarifu Francis Gachuri, kampeini za kujitwalia bendera zimeshika kasi, huku mawaziri walio kwenye baraza la sasa wakifanya juu chini kuhifadhi nafasi zao, licha ya fununu kuwa angalau tisa kati yao watapigwa kalamu.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: NEWSNIGHT | Kalonzo quizzed over claims of support for Uhuru term extension

Story By Francis Gachuri
More by this author