Wanasiasa waliohamia Jubilee watakiwa wajiuzulu

Wabunge na magavana wa CORD waliohamia chama kipya cha Jubilee wametakiwa kujiuzulu, na kutafuta mamlaka upya kupitia chama walichohamia. Kinara mwenza wa CORD Moses Wetang’ula amesema sheria ya vyama vya kisiasa ni bayana, kuwa huwezi kuwa mwanachama wa vyama viwili vya kisiasa kwa wakati mmoja. Msajili wa vyama Lucy Ndung’u anasisitiza hana mamlaka ya kuwaondoa kwenye sajili, wanachama wa vyama waliohamia Jubilee, bila ombi hilo kuwasilishwa kwake rasmi na vyama vilivyoathiriwa.

Tags:

JUBILEE CORD defectors

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories