Watu zaidi ya 300 waambukizwa kipindupindu Nairobi


Gavana wa Nairobi Evans Kidero amepiga marufuku wauzaji wote wa maji wa kibinafsi wanaotumia malori ya kuuzia maji jijini, akishikilia kuwa lazima wawe na idhini kutoka kwa kampuni ya maji ya Nairobi kabla ya kushiriki biashara hiyo.
Haya yanajiri huku kaunti ya Nairobi ikithibitisha kuwa watu wanne kati ya 336 walioripotiwa kuwa na kipindupindu jijini katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, wameaga dunia.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya watu 36 wakiwemo maafisa wakuu serikalini kuugua maradhi yanayodaiwa kuwa ni kipindupindu baada ya kula chakula katika jumba la kicc kwenye warsha ya kibiashara.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: | BULLDOZERS FOR SANITIZERS | Families remain in the cold after evictions from Kariobangi sewage estate

Avatar
Story By Hassan Mugambi
More by this author