Waziri Matiangi atoa hakikisho la usalama wa mitihani ya KCPE na KCSE

Waziri Matiangi atoa hakikisho la usalama wa mitihani ya KCPE na KCSE

Wizara ya usalama nchini imetoa hakikisho la usalama wa mitihani ya kitaifa na wanafunzi katika maeneo mbalimbali nchini.

Hakikisho hili limetolewa huku maafisa wakuu katika wizara ya elimu na baraza la mitihani wakihakikisha kuwa mikakati iko shwari kuhusu maandalizi ya mitihani ya KCPE NA KCSE mwaka huu.

Aidha, imebainika kwamba zaidi ya shule 200 zinachunguzwa kwa kushiriki njama ya kuiba mitihani hiyo.

Maelfu ya maafisa wa idara tofauti za élimu na usalama kote nchini walijumuika siku ya Jumatatu kwenye mkondo wa lala salama wa maandalizi ya mitihani ya kitaifa mwaka huu.

Waziri wa elimu Amina Mohammed mara hii akiwa mwenyeji wa mwenzake wa usalama Fred Matiang’i ambaye alioiongoza wizara ya elimu katika kipindi kilichopita.

Na walitoa mwelekeo kuhusu mikakati ya kuhakikisha kuwa hakuna visa vyoyote vinashuhudiwa.

Zaidi ya maafisa wa polisi 70,000 watapelekwa katika maeneo tofauti nchini kudumisha usalama. Mbali na hayo wafanyikazi 300 wa teknolojia ya mawasiliano pia watahusishwa.

Makamishna wa kaunti tofauti na wakuu wa elimu katika kaunti hizo walipokezwa kufuli na funguo zinazohifadhi karatasi za mitihani hiyo.

Aidha onyo kali ilitolewa kwa yeyote mwenye nia ya kuvuruga mitihani hiyo kwa kufungua karatasi hizo kabla ya wakati wake au hata kupatikana akisambaza karatasi ghushi kwa wazazi na wanafunzi.

Mitihani ya KCPE itaanza tarehe 30 mwezi huu huku KCSE ikianza tarehe 5 mwezi Novemba.

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories