Waziri wa sheria TZ, asutwa kwa kubuni sheria ya ndoa

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amebatilisha agizo la waziri wa katiba na sheria Dkt Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu. Akizungumza katika ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma magufuli amesema sharti hilo litawanyima Watanzania wengi haki ya kuoa au kuolewa kwa sababu hawana vyeti vya kuzaliwa. Raia wengi wa nchi hiyo walikuwa wamekera na agizo hilo huku wengine wakimtaka waziri Mwakyembe ajiuzulu. Mwanahabari wetu Samuel Mwalongo kutoka Dar-es-Salaam Tanzania anaarifu zaidi.

Tags:

Tanzania Rais John Pombe Magufuli Sheria ya ndoa

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories