Wizi wa mitihani : Shule ya St Theresa Girls Nakuru yafungwa

Shule ya upili ya kibinafsi ya st. Theresa senior, katika kaunti ya Nakuru imepokonywa cheti cha kuhudumu baada ya kupotikana na hatia ya  udanganyifu katika mtihani wa KCSE unaoendelea. Kupitia barua kwa usimamizi wa shule hiyo katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang’ ameamuru mwalimu mkuu kurejesha cheti cha usajili wa shule hiyo kwa mkurugenzi wa elimu wa kaunti ya Nakuru mara moja na kuifunga shule hiyo. Haya yanajiri huku waziri wa elimu Fred Matiangi akisema hakuna atakayesazwa iwapo atakiuka sheria.

Want to send us a story? SMS to 25170 or WhatsApp 0743570000 or Submit on Citizen Digital or email wananchi@royalmedia.co.ke

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories