Yadaiwa Ocampo alichelewesha kesi za ICC makusudi


Upekuzi wa hivi punde umebaini kuwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa (ICC) Luis Moreno Ocampo alifanya kila juhudi kuchelewesha maamuzi kuhusu mashtaka yaliyomkabili Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto na washukiwa wengine wanne ili kujiondolea fedheha kutokana na uchunguzi duni aliofanya. Upekuzi huo uliofanywa na muungano wa mashirika ya habari nchini ufaransa – Mediapart, umebaini kuwa Ocampo alimshawishi kiongozi wa sasa wa mashtaka ya umma Fatou Bensouda kutamatisha kesi ya Kenyatta, ili kujiondolea mzigo, na kujaribu kuikinga sura ya mahakama.

For Citizen TV updates
Join @citizentvke Telegram channelVideo Of The Day: | BULLDOZERS FOR SANITIZERS | Families remain in the cold after evictions from Kariobangi sewage estate

Avatar
Story By Francis Gachuri
More by this author